Skip to main content

KUPATWA KWA MWEZI

KUPATWA KWA MWEZI FUNZO LA SAYANSI

KUPATWA KWA MWEZI FUNZO LA SAYANSO

 12-3-2023


Tukio hili ni adimu katika karne hii kwani Mwezi utafunikwa kabisa na kivuli cha sayari yetu ya Dunia na mara ya mwisho tukio hili lilitokea miaka arobaini iliyopita tarehe 6/08/1971. Kipindi hicho wengu wetu tulikuwa hatujazaliwa na hata waliokuwepo ni wachache walioweza kutambua ni nini kilichokuwa kinaendelea.

Picha ya Kupatwa kwa Mwezi

Kupatwa huku kutatokea wakati mwezi ukiwa mpevu (full moon) ambapo mwezi utachomoza saa 12:03 jioni kabla ya jua kuzama na masaa matatu baadae saa 3:22 usiku upande wa mashariki wa mwezi utaanza kupokea taratibu kuvuli cha sayari ya Dunia.

Baada ya lisaa limoja saa 4:22 usiku mwezi mzima utakuwa umemezwa katika kivuli cha Sayari ya Dunia na hapa ndio utakuwa mwanzo wa kupatwa kamili kwa mwezi (Total Lunar Eclipse). Mwezi utapita katikati ya kipenyo cha kivuli cha sayari ya Dunia na ifikapo saa 5:02 usiku utakuwa katikati ya kivuli kinene cha sayari Dunia na kusababisha kiza kinene kinachoashiria kupatwa kamili kwa mwezi kama ilivyokuwa miaka 40 iliyopita.

Mwezi utakuwa umezingirwa katika kivuli cha sayari ya Dunia hadi saa 6:03 na baada ya hapo sehemu ya upande wa mashariki ya mwezi itaanza kutoka katika kivuli cha Dunia na tukio hili litaendelea kwa lisaa limoja hadi saa 7:02 usiku ambapo mwezi utakuwa umeondoka katika kivuli cha Dunia na kurudia katika hali yake ya kawaida.

Picha ya kuonyesha mda wa kupatwa kwa Mwezi

Tukio hili la pekee ni funzo la sayansi kwa watoto, wazazi na jamii yote kwa ujumla kwani wengi wetu hatufahamu wala kuamini kama ni kweli Dunia inaelea na kuzunguka Jua na pia ni vigumu kwetu sisi kufahamu jinsi mwezi unavyoizunguka sayari ya Dunia.

Kutokana na tukio hili tunaweza kujiuliza maswali mengi na kuhisi ni jinsi gani tulivyo na uhusiano wa karibu na anga yetu. Kupatwa kwa Mwezi hutokea pindi sayari ya Dunia, Nyota ya Jua na Mwezi vinapokuwa katika mstari mmoja vikiwa katika mizunguko yake.

Sayari ya Dunia inazungukwa na Mwezi kwa siku takribani 27 au 29 na kufanya mwezi mmoja wa kalenda na Mwezi pamoja na Dunia vinazunguka Jua kwa siku takribani 365 na kufanya mwaka mmoja wa kalenda. Dunia na Mwezi vinazunguka jua katika nyuzi (angle) mbali mbali na kusababisha matukio ya kupatwa kwa Mwezi na Jua kutokea mara chache.

Jua ni chanzo pekee cha mwanga katika mfumo wa Jua hivyo na hivyo hutengeneza kuvuli kwenye uso wa Mwezi pale sayari yetu inavyokatiza katikati yake na mwezi katika mstari ulio nyooka na kufanya tuone kivuli cha sayari yetu kwenye uso wa mwezi. Hii inadhihirisha kwamba sisi na Sayari yetu tupo kwenye mwendo siku zote za maisha yetu na nguvu ya uvutani (Universal Gravitational Force) ndio inatushikilia hapa tulipo.

NB: Baadhi ya maneno yametafsiriwa kutoka kwenye Makala ya Dr. Jiwaji iitwayo Darkest Total Luna Eclipse 14/06/2011 na pia picha ya mda wa kupatwa kwa Mwezi imetolewa huko.

Comments

Popular posts from this blog

Aua kisa cheo

MWALIMU ADAIWA KUUA MWALIMU MWENZAKE KISA CHEO... Mwalimu wa Shule ya Msingi Igaka, Samwel Subi anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Geita kwa tuhuma za kumuua mwalimu mwezake Emanuel Chacha (pichani) kwa kumchoma na kisu akiwa darasani. Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema limetokea Machi 15 saa 3:45 asubuhi wakati walimu hao wakiandaa mtihani kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la kwanza. "Kata ya Isulwabutundwe mwanaume wa miaka 35 katika Shule ya Msingi Igaka aliuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kwenye chembe ya moyo na mwanaume mwingine mwenye miaka 35 ambae ni mwalimu mwenzake. Walimu wote wawili walikuwa darasani wakiandaa mtihani ndipo mtuhumiwa alitoa kisu na kumchoma mwenzake kwenye chembe cha moyo," amesema Kamanda Jongo. Kamanda alisema chanzo cha tukio hilo inadaiwa kuwa ni ugomvi baina ya walimu hao ambao walikuwa wanagombea uongozi kwenye kitengo cha elimu ya kujitegemea. "Uchunguzi wa tukio hilo...

JE NI UGONJWA AU ULEVI?

Pichani ni Methew Hogg Raia wa Uingereza ambaye ana ugonjwa unaoitwa auto-Brewery Syndrome.  Ugonjwa huu ni kwamba Mwili wake una uwezo wa kutengeneza Pombe wenyewe endapo tu atakula chakula chenye Sukari au Wanga.  Hogg anasema endapo atakula Sahani Moja tu ya wali Mwili wake hutengeneza pombe yenye kiwango cha Chupa tatu za Wine kali kabisa. Jamaa kila siku huamka na hungover ya kufa mtu.  Akiwa mdogo alikuwa hajaelewa kuhusu ugonjwa huu hivyo akiwa shuleni alikuwa akilewa hovyo hovyo pindi anapokula chakula chenye wanga, sukari au Amira.  Fuata link hii kumsoma zaidi. Pombe inayotengenezwa tumboni kwa jamaa wanasema ni kali sana. Picha ya pili hapo ni kwamba jamaa anataka kulewa akila huo mkate

Watering simply

 Project of watering system at your home do it's try it it save water                  https://youtu.be/nEVqE09aRvA 👆 It's just simple to do just like  Look video here 👇 https://youtu.be/nEVqE09aRvA To have fire  Needle