Skip to main content

Aua kisa cheo



MWALIMU ADAIWA KUUA MWALIMU MWENZAKE KISA CHEO...

Mwalimu wa Shule ya Msingi Igaka, Samwel Subi anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Geita kwa tuhuma za kumuua mwalimu mwezake Emanuel Chacha (pichani) kwa kumchoma na kisu akiwa darasani.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema limetokea Machi 15 saa 3:45 asubuhi wakati walimu hao wakiandaa mtihani kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la kwanza.

"Kata ya Isulwabutundwe mwanaume wa miaka 35 katika Shule ya Msingi Igaka aliuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kwenye chembe ya moyo na mwanaume mwingine mwenye miaka 35 ambae ni mwalimu mwenzake. Walimu wote wawili walikuwa darasani wakiandaa mtihani ndipo mtuhumiwa alitoa kisu na kumchoma mwenzake kwenye chembe cha moyo," amesema Kamanda Jongo.

Kamanda alisema chanzo cha tukio hilo inadaiwa kuwa ni ugomvi baina ya walimu hao ambao walikuwa wanagombea uongozi kwenye kitengo cha elimu ya kujitegemea.

"Uchunguzi wa tukio hilo unaendelea mwalimu amekamatwa na amekiri na sababu anadai aliona walimu wenyeji wanamchukia na wamemtenga na ndio sababu ya kutengeneza nia ya kutenda tukio hilo," amesema.

Source: Mwananchi

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA ZILIZOVUNJA REKODI\ THE STORY MAKE HEADLINES

Source Google Pic edition Wedish warship Vasa. It sank in 1628 less than a mile into its maiden voyage and was recovered from the sea floor after 333 years almost completely intact. Now housed at the Vasa Museum in Stockholm, is the world's best preserved 17th century ship            Swahili Meli ya KIVITA ya kiswiden\ swidish. Kwa jina. Vasa iliyozama takribani 1628 zaidi ya maili chini ya bahari katika eneo la matengenezo na ilidumu ndani ya bahari takribani miaka 333         Kwa Sasa imejengewa eneo kama makumbusho huko Stockholm.  Ni Moja kati ya rekodi za Dunia tangia Karne ya 17 katika meli za nchi hiyo ya sweden     

MALKIA WA GIZA

Lugha ya kiswahili Kutana na mwana mitindo Kwa jina  Nyakim Gatwech,    Mwanamke mweusi zaidi Duniani Jina alilokubaliananalo mwanadada ambaye pia ni mwanamitindo mwenye asili ya Sudan mwanamadada hiyo ambaye muonekano wake umekuwa hivyo kutokana n mlimbikizo au wingi wa melanin ambazo ni Kinga za ngozi zinazoratibu ukoleaji wa rangi ya mwili na kuilinda dhidi ya miale ya jua     Licha ya hayo mwanamke hiyo ni balozi wa wanawake weusi anawahasa watu wasiogope GIZA kwakuwa hata watu weusi ni watu kama watu wengine tofauti ni rangi tua     Pia anawahasa watu hasa wanawake kujikubali kwakuwa weusi ni urembo ulioumba na Mungu       Kwa Sasa mwanamke hiyo anaishi nchini marekani kwashughuli za mitindo ambayo ndiyo maisha yake Kwa ujumla     Kwa ujumla unapaswa kukipenda namna Mungu alivyokuumba  Jipende tu haijalishi umeumbwa Kwa staili gani kubaliana na uumbaji wa Mungu Kila kitu ni mpango wake       Picha ...